text
stringlengths 0
4.5k
|
---|
Wametaja baadhi ya mahitaji yao muhimu kwa sasa kuwa ni pamoja na Sare za shule kutokana na kuchakaa kwa sare wanazotumia ikiwemo Madaftari, kalamu,Masweta, Viatu, mafuta ya kupikia, mafuta ya kupaka, sabuni, chumvi, mkaa, Unga, Mchele na maharage. |
VIJANA WAJA NA MAPENDEKEZO MABORESHO SERA YA TAIFA YA VIJANA |
Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bw. Suleiman Makwita akiwasilisha muhtasari wa uchambuzi wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) akiwa pamoja na baadhi ya wananchama wa asasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya wananchama wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) wakifuatilia muhtasari wa uchambuzi wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 uliokuwa ukiwasilishwa mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) na Mwenyekiti wa Asasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. |
Wanachama wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kuwasilisha muhtasari wa uchambuzi wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. |
Asasi za Kiraia za zinazounda Umoja wa AZAKI za juu ya masuala ya Bunge kwa kushirikiana na asasi zingine waja na mapendekezo katika kuboresha Sera ya Taifa ya Vijana ya mwaka 2007 ili iendane na wakati pamoja na mabadiliko ya kiteknolojia. |
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) ambayo ni Asasi kiongozi Bw. Suleiman Makwita wakati akiwasilisha muhtasari wa uchambuzi wa Sera hiyo. |
Makwita amesema kuwa lengo la kufanya mapitio juu ya Sera hiyo ni kuangalia namma ambapo wanaweza wakaishauri Serikali maeneo ya kufanyia maboresho katika Sera hiyo ya vijana. |
“lengo la kufanya uchambuzi huu ni kuiomba Serikali na wadau wote wa maendeleo ya vijan nchini kuweka mazingira rafiki yatakayochochea maeneleo ya vijana kupitia sekta rasmi na zisizo rasmi ikijuisha masuala mtambuka na kuendana na dhana ya maelengo endelevu ya dunia” alisema Makwita. |
Akizungumzia matokeo ya uchambuzi huo Makweta alisema kuwa wamebaini baadhi ya changamoto zilizopo katika Sera ya Vijana ya Mwaka 207 na hatimaye wamekuja na baadhi ya mapendekezo kama njia ya kusaidia kuiboresha Sera hiyo. |
Baadhi ya mapendekezo waliyokuja nayo ni pamoja na kuanishwa kwa umri wa kijana kuwa miaka 13 -35 tofauti na sasa ambapo kijana anatambuli kuwa na umri kati ya 15 hadi 35. |
Aliongeza kuwa katika masuala ya afya Sera inapaswa kukugusia masuala yote yanayoathiri vijana kama vile afya ya uzazi, anemia,TB na Selimundu, badala ya kutilia mkazo kwenye VVU/Ukimwi pekee. |
Pamoja na mapendekezo hayo Makwita aliipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa vijana kijana, pamoja nakufanyia kazi baadhi ya mapendekezo ya wadau mbalimbali ikiwemo kuanzishwa kwa Baraza la Taifa la Vijana. |
hivyo vitabu vya dini sasa sivielewi lakini kumbuka viliandikwa na watu pia kama wewe, yasinta au mbele. |
Nimekutana na mjadala huu kwa mara ya pili, ambapo debate ilikua hii hii ya masuala la mshahara kutosha au kutokutosha.Katika mada hiyo ndipo ilipoibuka hoja ya Kufanya kazi kwa bidii kama njia ya maendeleo, ambayo ni hoja yako ya msingi. |
Ahsante sana kwa kunitembelea na kutuelimisha. |
nakubaliana na wewe kwa mtazamo wako na pia nakubaliana na Kamala kwa mtazamo wake. |
Lengo langu lilikuwa ni kuweka ule mjadala katika hali ya kukosoana bila kujeruhiana kwa maneno ya kuzodoana. |
Nakubali kuwa kuna dhulma nyingi katika nchi hii, lakini hebu tujiulize mimi na wewe, Je hiyo inahalalisha uzembe na kutokufanya kazi? |
Hivi ni nani anawachagua hawa viongozi tulio nao leo tena kwa kura za kishindo? |
Kwangu mimi, naona hii ni changamoto kwa jamii, kukaa na kujiuliza, hali hii mapaka lini? |
Je kuna haja ya kuendelea kukumbatia uozo huu ambao hauna manufaa kwetu na badala yake unatuumiza? |
Bado nasisitiza kuwa kuna haja ya jamii kubadilika na kufanya kazi, tena kwa bidii, ili kujiletea maendeleo na kama ni swala la serikali kutokuweka sera zitakazolinda maslahi ya wananchi wake basi mwaka 2010 sio mbali, tuwaondoe. |
Watu wa Musoma wametuonesha kuwa inawezekana, isiishie huko, kama wote tukiamua na kusema basi inatosha, hakika inawezekana. |
kazi kuilaumu serikali utafikiri wewe sio sehemu ya serikali. naomba majibu ya maswali ili mada inoge zaidi labda. |
Mwandishi wa habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, Amina Athuman (pichani) amefariki Dunia leo asubuhi katika Hosptali ya Mnazi Mmoja mjini Zanziba alikokuwa amelazwa. |
Amina alilazwa Hospitalini hapo baada ya kuzidiwa (kushikwa na uchungu) kutokana na ujauzito na kukimbizwa kupata huduma katika hospitali hiyo ambpo alijifungua mtoto wa Kiume (Bahati mbaya) na yeye akaendelea kupatiwa matibabu hadi ulipomkuta umauti asubuhi ya leo. |
Amina alikua mjini Zanziba kikazi alipokwenda kuripoti mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo alikuwa arejee jijini Dar es Salaam jana. |
Sikukuu ya Wafanyakazi |
Siku ya Kumbukumbu ya Karume |
Profesa Thornton ameyasema hayo leo (Jumatano) Ikulu alipokutana na Rais John Magufuli kwa ajili ya kujadiliana kuhusu sakata la mchanga wa madini. |
Hakuna tatizo tumia fomu yetu ya kupata nywila na kuingiza tena. |
Umesahau nywila yako |
HABARI NI HABARI NDUGU YANGU: Chadema na ushindi wa kujivunia |
@Uwanja wa Jamhuri, Mkoani Dodoma |
Wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa jirani wanakaribishwa kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa mwaka huu ambayo yanatarajia kufanyika kitaifa Mkoani Dodoma. Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo ni “Uhuru wetu ni Tunu, Tuudumishe, Tulinde Rasilimali zetu, Tuwe Wazalendo, Tukemee Rushwa na Uzembe”. |
KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATANO MEI 16, 2018 |
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma: Commonwealth Secretariet Vacancy Announcement |
Rais Magufuli Atoa Wito kwa Nchi Wanachama Kusimamia Vyema Rasilimali Walizonazo. |
Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya mabadiliko kidogo ya timu zilizo kwenye makundi ya ‘A’ na ‘B’ katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Septemba 16, mwaka huu. |
Timu ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Polisi Morogoro FC ya Morogoro iliyokuwa kundi ‘A’ sasa itakuwa Kundi ‘B’ wakati Mshikamano FC ya Dar es Salaam iliyokuwa Kundi ‘B’ sasa itacheza mechi mechi zake katika Kundi ‘A’. |
Kwa msingi huo, makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila kund, zitakazochuana msimu huu wa 2017/18 kuwania nafasi tatu muhimu za kupanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2018/19 yatakuwa hivi:- |
Kundi ‘A’ litakuwa na timu za African Lyon, Ashati United, Friends Rangers, Mshikamano za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga na Mvuvumwa ya Kigoma. |
Mji wa Longido Kupata Majisafi na Salama kwa Asilimia 100 |
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi. Irina Bokova, katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo ametaka wananchi mbalimbali kutenga muda binafsi na kutembelea moja ya maeneo ambayo ni urithi wa dunia yakifadhiliwa na UNESCO. |
Amesema anaamini kuwa kwa wananchi kushiriki watashawishika kuendelea kuishi kwenye maeneo hayo na kuyaenzi. |
Amesema kitendo hicho kidhati kitakuwa kimewaunganisha watu na asili na hivyo kuondoa dhana ya zamani ya kuweka maeneo hayo mbali na watu. |
“Inaweza kuwa vigumu kuamini sasa, lakini miaka hamsini iliyopita ilidhaniwa kuwa njia bora ya kulinda asili ni kuiweka mbali na watu ...Hii leo, tunajua vyema zaidi kwamba kwa kadri uhusiano baina ya watu na mazingira yao unavyokuwa wa karibu zaidi ndivyo watu wanavyofahamu zaidi juu ya umuhimu wa asili na viumbe hai, urithi na maji, kwa ajili ya ustawi wao binafsi na kwa ajili ya hali ya baadaye ya sayari yetu.” Alisema. |
Mkuu huyo alisema hayo akizungumzia umuhimu na uhifadhi kwa maeneio zaidi ya 2000 duniani ya bayongahewa, maeneo ya hifadhi ya jiolojia ya na maeneo ya Urithi wa Dunia yanayodhaminiwa na UNESCO. |
Alisema maeneo hayo pamoja na kuhifadhi urithi wa dunia pia hutoa ajira kwa watu wanaoyazunguka na milango yake iko wazi kwa umma wote. |
“Maeneo ya hifadhi ya jiolojia ni vitabu vilivyo wazi vya kihistoria ambavyo huturudisha nyuma mamilioni ya miaka. Hifadhi za Bayongahewa ni mahali ambapo jamii hukabiliana na changamoto za maendeleo kwa kuunda njia mpya za kijamii na uchumi endelevu. Maeneo ya hifadhi ya jiolojia na hifadhi za Bayongahewa huunganisha uhifadhi na elimu kwa mbinu mpya ya maendeleo endelevu, kama vile utalii wa mazingira na kilimo hai.” alisema katika ujumbe wake kwa dunia. |
Aidha alisema vyema kuona eneo la hifadhi ya jiolojia la UNESCO la Tumbler Ridge nchini Canada, na kuogelea katika maziwa ya Alpine yenye maji angavu kama kioo na kulala chini ya nyota. |
Pia amewataka kufanya safari ya kutembea kwa miguu katika hifadhi ya Bayongahewa ya Mujib huko Jordan ambayo ipo mita 420 chini ya usawa wa bahari ikiwa karibu wake na Bahari ya Chumvi. |
Mkuu huyo wa Unesco ametaka wakazi wa dunia hii wakati wakiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, kutumia ipasavyo maeneo teule ya UNESCO kila mahali kuungana na asili inayowazunguka na inayoleta uzuri, maana na amani katika maisha. |
Sifa "Kila kitu kinachoelezewa" kinatangaza Ufaransa Inter kuhusu matumizi ya hidrojeni na matumizi yake ya nishati. |
Pakua faili (usajili wa jarida inaweza kuhitajika): Ufaransa-Inter: kila kitu kinafafanuliwa juu ya hidrojeni |
Taswira: Ziara ya Msajili wa Vyama Jaji Mutungi Ofisi za CHADEMA Kanda ya Kaskazini |
Jaji Mutungi amesema kuwa ANAPENDELEA KUWA KARIBU NA VYAMA VYA SIASA YEYE KAMA MLEZI jambo ambalo litasaidia kujua uhitaji wa vyama Vya Siasa na hata kutoa ushauri kwao. |
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi akizungumza na viongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini katika ofisi ya Kanda eneo la Ngarenaro Jijini Arusha |
Taswira: Ziara ya Msajili wa Vyama Jaji Mutungi Of... |
Baada ya Kushika Nafasi ya Kwanza Kwa Usafi, Jiji ... |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Aamuru Wananchi wa Kijiji Kizima Wakamatwe na Kuwekwa Ndani…..RPC Mbeya Tayari Keshatuma Polisi |
Kampuni ya Uber yapata Mkurugenzi Mtendaji mpya. Dara Khosrowshashi, mmarekani mwenye asili ya Iran amekuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni ya usafiri ya Uber. |
Khosrowshashi ambaye alikuwa mtendaji mkuu wa kampuni ya huduma za usafiri mtandaoni ya Expedia, Jumanne iliyopita alithibitisha kuwa angekubali nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Uber. |
Khosrowshashi alitangaza nia yake ya kuchukua uongozi wa kampuni ya usafiri ya Uber yenye makao makuu yake huko San Francisco alipofanya mahojiano na Wall Street Journal na Bloomberg. |
Bodi ya wakurugenzi wa Uber walipiga kura Jumapili usiku kumpendekeza Khosrowshashi. |
Mwaka huu wa 2017, Uber imehusishwa na kashfa kuhusiana na madai ya watendaji wake kuunga mkono utawala wa Rais Donald Trump na mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsia katika makao makuu ya kampuni hiyo. |
Ushirikiano wa Uber na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Trump, Travis Kalanick, uliacha kampuni hiyo mwezi Juni katika wakati mgumu. |
Lakini Kalanick atabaki kwenye bodi ya Uber na anamiliki kiasi kikubwa cha hisa za kampuni hiyo. Kwa sasa ameshtakiwa na mwanachama mwingine wa bodi ya Uber, Benchmark Capital Partners, ambaye anamshtaki kwa udanganyifu. |
Kupitia jarida la Los Angeles Times, Msemaji wa Kalanick ametupilia mbali madai hayo , akisema kuwa mashtaka hayo hayakuwa ya ukweli na yamejaa uongo. |
Ingawa Uber imepunguza hasara kwa kipindi cha robo ya mwaka, lakini imepoteza dola 645 milioni kwa mapato ya dola 1.75 bilioni wakati wa robo ya pili ya mwaka huu. |
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bi Joyce Mkinga (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kufanyika kwa Mkutano wa Maafisa Mipango unaotarajiwa kufanyika Mwezi wa Oktoba mwaka huu. Kulia ni Mchumi Mkuu (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Omary Juma. |
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ipo katika maandalizi ya mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango unatarajiwa kufanyika Oktoba 2014 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na usimamizi wa uchumi na mipango hapa nchini. |
Mkutano huu ambao ni wa kitaalamu unawakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka tasnia za mipango, uchumi, takwimu na maendeleo, wenye wajibu wa kusimamia uchumi na mipango ambao hukutana kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya sera, mipango na kujenga mtandao wa masuala ya maendeleo ya kitaaluma. |
Mkutano huu unatoa fursa kubwa ya kuwakutanisha kwa pamoja wataalamu hao na kujenga uelewa wa pamoja juu ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Serikali. Pia hutoa fursa za kujadiliana kwa pamoja juu ya mafanikio na njia za kukabiliana na changamoto kwa kubadilishana uzoefu na ujuzi kwenye masuala hayo. Mkutano huo ni muhimu katika kuimarisha utendaji kazi wa kada hizi kwa minajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. |
Kwa kutilia mkazo masuala mbalimbali ya kimaendeleo yanayojitokeza hivi sasa, mkutano wa mwaka huu utajikita katika kujadili masuala yafuatayo; |
Mkutano utajadili fursa, na changamoto zilizopo katika kuleta maendeleo katika nchi. Huko nyuma kada hizi zilikuwa zinaratibiwa na iliyokuwa Wizara ya Mipango Uchumi na Uwezeshaji. Kwa sasa watakuwa chini ya uratibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Hatua hii itarahisisha utekelezaji wa mipango mbalimbali ya nchi. |
Utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Maendeleo 2011/12 – 2015/16) unaendelea na tayari Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango imeanza kufanya mapitio ya utekelezaji wake ili kujua mafanikio na changamoto. Hivyo, katika mkutano huo wapanga mipango wanaandaliwa waweze kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya Mpango wa Pili wa Maendeleo (2015/16 – 2020/21). |
iii) Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika Sekta ya Umma; |
Serikali imeandaa mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika sekta ya Umma, lengo likiwa kuimarisha utendaji, ufanisi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya miradi na program za maendeleo. |
iv) Jinsi ya Kujiandaa na Uchumi wa Gesi |